Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Balozi mwema wa UNICEF David Beckham aleta sauti za watoto kwa UM

Balozi mwema wa UNICEF David Beckham aleta sauti za watoto kwa UM

Leo kwenye Umoja wa Mataifa, kimezinduliwa chombo cha aina yake kinacholeta sauti za watoto na vijana kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, katika hafla iliyoongozwa na Balozi Mwema wa Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF, David Bekcham, Katibu Mkuu Ban Ki-moon na Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Anthony Lake.

Chombo hicho cha dijitali kilichoundwa na kamopuni ya Google, kinaunganisha teknolojia ya simu za mkononi na mitandao ya kijamii ili kuwawezesha watoto na vijana kote duniani kutuma ujumbe wao moja kwa moja kwa viongozi wa dunia.

Ujumbe wa watoto hao unamulika changamoto wanazokumbana nazo nyumbani na katika jamii, zikiwemo umaskini uliokithiri, utofauti, ukatili, magonjwa na mizozo, huku wakielezea matumaini ya mustakhbali wao. Hapa, ni David Beckham akitoa ujumbe wake

“Kila mtoto ana sauti, lakini mara nyingi, hawasikiki. Wakati huu muhimu viongozi wa dunia wanapokusanyika hapa New York, sauti zao zitasikika. Dunia inapoangazia malengo mapya ya dunia, kuna fursa halisi ya kutimiza ndoto zao. Nataka ulimwengu ambapo watoto wanaweza kukua salama bila ukatili, bila umaskini na kulindwa kutokana na maradhi yanayoweza kuzuiliwa”