Skip to main content

Kilimo hai na utalii vyaweza kupunguza umaskini Tanzania:UNCTAD

Kilimo hai na utalii vyaweza kupunguza umaskini Tanzania:UNCTAD

Ripoti mpya ya kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa, UNCTAD imesema kilimo hai na utalii vikifanyika kwa pamoja vinaweza kukwamua Tanzania kutoka lindi la umaskini. Taarifa kamili na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Ikiitwa kuimarisha uhusiano kati ya sekta ya utalii na kilimo nchini Tanzania, ripoti hiyo iliyotolewa leo imetokana na ufinyu wa utafiti wa sera za utalii zinazoinua maskini na hivyo ripoti inaainisha fursa za kuendeleza ushiriki wa sekta binafsi katika ubia na wakazi wa vijiini.

Mathalani kupitia sera bora, sekta binafsi inaweza kuanzisha hoteli ambazo kwazo wakazi wa eneo husika wanaweza kuuza bidhaa zilizozalishwa kwa njia ya kilimo hai, mazao ambayo yanapendwa zaidi na watalii na bei yake ni ya juu.

Hata hivyo ripoti hiyo imetaka kuwepo kwa mawasiliano ya moja kwa moja kati ya wauzaji na wanunuzi wa mazao hayo kwani ushahidi umeonyesha kuwa hata sasa mazao hayo licha ya kuzalishwa kwa wingi, ukosefu wa mawasiliano ya moja kwa moja kati ya pande mbili hizo, unakwamisha maendeleo ya sekta ya kilimo hicho.