Skip to main content

Malengo ya Maendeleo Endelevu yaangaziwa

Malengo ya Maendeleo Endelevu yaangaziwa

Leo ikiwa ni mapumiziko kwenye Umoja wa Mataifa kusherehekea sikukuu ya Eid Al Haji tunamulika malengo ya maendeleo endelevu SDG au ajenda 2030,  ambayo itaridhiwa rasmi mwisho wa wiki hii hapa New York Marekani.

Katika mkutano huo wa ngazi ya juu ambapo viongozi wa dunia wanatarajiwa kushiriki wakiwemo Kiongozi wa kanisa katoliki duniani , Papa Francis na marais wa nchi za Afrika Mashariki na wengineo,  malengo mapya 17 yatapitishwa ambayo yataongoza kazi ya Umoja wa Mataifa na serikali za nchi wanachama katika shughuli za maendeleo kwa kipindi cha miaka kumi na mitano ijayo.

Ajenda 2030 au SDG itachukua nafasi ya malengo ya maendeleo ya milenia yaani MDG ya mwaka 2000 yanayofikia ukomo wiki hii.

Tukiwa tunafungua ukurasa wa malengo mapya yaani SDGs, utekelezaji wa malengo ya milenia unaelezwa kuwa na mafanikio licha ya changamoto kadhaa hususani barani Afrika mathalani nchini Kenya ambapo wananchi wanasema mengi yanahitajika kufanyika kama walivyoongea na redio washirika KBC.

 (VOX POP)

Balozi wa kudumu wa Kenya katika Umoja wa Mataifa Machariya Kamau ni mwenyekiti mwenza wa kikosi kazi kilichoratibu mchakato wa kuandaa malengo 17 ya maendeleo andelevu au agenda 2030 amemweleza Joseph Msami kinagaubaga juu ya uanzishwaji wa malengo hayo.

(Balozi Kamau)

(MIDWAY STING)

Unasikiliza jarida maalum msikilizaji leo ikiwa ni mapumziko kwenye Umoja wa Mataifa, tunaangazia malengo mapya ya maendeleo endelevu SDGs yatakayokuwa dira ya dunia katika maendeleo kwa kipindi cha miaka 15 ijayo.

Nicolo Gnecchi ni mtalaam wa mawasiliano kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo au UNDP ambalo limekuwa na mchango mkubwa katika utekelezaji na uundaji wa malengo hayo.

Ameongea na Priscilla Lecomte kuhusu SDGs akianza kwa kueleza mchango wa UNDP ni upi.

(Sauti Nicolo)