Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalam wa UM kutathmini hali ya wahamiaji Australia

Mtaalam wa UM kutathmini hali ya wahamiaji Australia

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za wahamiaji, François Crépeau, atafanya ziara nchini Australia kuanzia Septemba 27 hadi Oktoba 9, 2015, kufanyia tathmini8 programu za uhamiaji, sera na sheria zilizoundwa na Australia katika miaka ya hivi karibuni.

Akitangaza ziara hiyo kwanza ya kukusanya taarifa nchini Australia, Bwana Crépeau amesema kuelewa jinsi Australia inavyodhibiti sera zake za uhamiaji na athari zake kwa haki za binadamu za wahamiaji kutakuwa sehemu muhimu ya ziara yake.

Katika ziara hiyo ya siku 13 nchini Australia, mtaalam huyo huru atakutana na maafisa kadhaa wa serikali wanaohusika na udhibiti wa mipaka, asasi za kiraia, vyama vya wafanyakazi, tume ya kitaifa ya haki za binadamu, mashirika ya kimataifa, na wahamiaji wenyewe, ili kujadili udhibiti kanganyifu wa mipaka ya Australia.

Ripoti ya ziara hiyo itawasilishwa kwa Baraza la Haki za Binadamu mnamo Juni 2016.