Skip to main content

UNAMID yaelekea kutimiza vigezo vyake, licha ya changamoto- Abdul Kamara

UNAMID yaelekea kutimiza vigezo vyake, licha ya changamoto- Abdul Kamara

Naibu Mkuu wa Ujumbe wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika huko Darfur, Sudan, UNAMID, amesema kuwa ujumbe huo umejitahidi kuboresha utendaji kazi wake katika kuwalinda watu wa Darfur, licha ya changamoto kubwa. Taarifa kamili na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Katika mahojiano na Radio UNAMID, Bwana Abdul Kamara, ambaye anaondoka baada ya kuuhudumia ujumbe wa UNAMID kwa muda wa mwaka mmoja, amemulika suala la vikosi kutotenda vyema kazi, ambalo Sudan imekuwa ikilalamikia, akisema suala hilo sasa limeshughulikiwa ipasavyo.

Ameongeza kuwa kwa kulishughulikia suala hilo, UNAMID imechukua hatua kali za kuviondoa vikosi ambavyo vilishindwa kutekeleza majukumu yao ya kuwalinda raia dhidi ya hali ya hatari.

Kuhusu changamoto zinazoikabili UNAMID, Bwana Kamara amesema vizuizi vya serikali ni changamoto inayozuia utendaji kazi kikamilifu kwa ujumbe huo, akitaja hatua ya serikali kukataa kutoa visa kwa waajiriwa wapya wa UNAMID kama mfano.