Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa Ulaya waipe umuhimu ajenda ya wakimbizi na wahamiaji: UNHCR

Viongozi wa Ulaya waipe umuhimu ajenda ya wakimbizi na wahamiaji: UNHCR

Wakati viongozi wa bara Ulaya wakikutana mjini Brussels Ubelgiji leo na kesho, Shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi UNHCR, limewataka viongozi hao kuungana dhidi ya dharura ya janga la wakimbizi na wahamiaji ambalo linaongeza machafuko na lisilotabirika.Taarifa kamili na Abdullahi Boru.

(Taarifa ya Abdullahi)

Kwa mujibu wa UNHCR, hii ni fursa ya mwisho kwa kwa bara Ulaya kushughulikia janga hili ambalo linaongeza mateso na unyanyasaji kwa wakimbizi na wahamiaji pamoja na kusababisha mivutano baina ya nchi.

Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa wa UNHCR António Guterres, janga hili ni la utashi wa kisiasa linalotokana na ukosefu wa Umoja baina ya nchi za Ulaya jambo linalosababisha ghasia akitolea mfano wa raia wa Hungary takribani 200,000 waliokimbilia Austria na Yugoslavia mwaka 1956 ambao walipokelewa vizuri na utaratibu wa kuwahamishia wengine 140,000 katika nchi nyingine ulifanyika hima.

Melissa Flaming ni msemaji wa UNHCR

‘‘Tunaamini kwamba katika mipango wanapaswa kuzingatia kuwa makumi ya maelfu ya wakimbizi na wahamiaji watahitaji malazi, na misaada mengine katika maeneo haya ya kuwapokea kwa wakati .’’