Wanawake na watoto kutoka Iraq wapatiwa makazi Ujerumani:IOM

22 Septemba 2015

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limewezesha wanawake na watoto 65 kutoka Dohuk na Erbil Iraq kupatiwa makazi huko Ujerumani.

Hatua hiyo ni sehemu ya mpango unaofadhiliwa kwa pamoja na serikali ya Ujerumani na IOM ukiwa na lengo la kuona wahanga wa mzozo wa Iraq walio hatarini zaidi wanapatiwa hifadhi Ujerumani.

Msemaji wa IOM Itayi Viriri amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kuwa mpango huo umeanza mwezi Machi mwaka huu na hadi sasa umenufaisha wairaq 329 na kwamba..

(Sauti ya Itayi)

“Sehemu ya mpango huu inahusisha wale ambao walijikuta moja kwa moja kwenye mzozo wakati mji wa Mosul ulipotwaliwa na ISIL na matarajio yetu ni kwamba tutakuwa tumehamisha watu wapatao Elfu Moja kwenda Ujerumani ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter