Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanachama wa Baraza la Usalama la UM Wapongeza washikadau wa kisiasa nchini Guinea Bissau

Wanachama wa Baraza la Usalama la UM Wapongeza washikadau wa kisiasa nchini Guinea Bissau

Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamepata taarifa ya uteuzi wa tarehe 17 Septemba 2015, wa Carlos Correia, wa Makamu wa Rais wa Kwanza wa Chama cha African Party for the Independence of Guinea and Cape Verde, PAIGC chama kikubwa cha kisiasa katika Bunge, kuwa Waziri Mkuu wa Guinea Bissau.

Katika taarifa, wanachama wa Baraza la Usalama walisisitiza uteuzi huo kama hatua muhimu katika kukomesha mgogoro wa kisiasa ambao umetanda nchini humo tangu katikati ya mwezi Agosti mwaka 2015.

Halikadhalika Wanachama hao walisisitiza umuhimu wa uundwaji wa serikali mpya haraka iwezekanavyo kwa kuheshimu utaratibu kamili za kikatiba.

Aidha, wamepongeza kuheshimiwa kwa Katiba na utawala wa kisheria ulionyeshwa na washikadau nchini Guinea Bissau ikiwa ni pamoja na kutoingiliwa kwa vyombo vya usalama katika hali ya kisiasa nchini humo na kujizuia kwao kulivyodhihirishwa katika suala hilo.