Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

McDonald's na Mashirika mengine yashiriki kwenye kampeni ya kuunga mkono WFP

McDonald's na Mashirika mengine yashiriki kwenye kampeni ya kuunga mkono WFP

Leo ikiwa ni siku ya Amani Duniani, mashirika ya sekta binafsi yameshirikiana kwa ajili ya kusaidia jitihada za Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula(WFP). Taarifa kamili na Abdullahi Boru..

(Taarifa ya Abdullahi)

Lengo la ushirika huo wa sekta binafsi ni kusisitiza umuhimu wa usaidizi wa chakula katika kukuza amani duniani, mkuu wa WFP, Ertharin Cousin akieleza kwamba wakati wa shida msaada wa chakula unaweza kurejesha matumaini, na kupunguza hatari ya mapigano.

Mashirika hayo ni pamoja na McDonald's, Burger King, Facebook, Google, Twitter na mengineyo, ambayo yanatangaza video ya sekunde 30 ya WFP kuhusu uhusiano kati ya vita na njaa. (Video inapatikana hapa : www.wfp.org/peace)

Pesa zitakazopatikana zitafadhili operesheni za WFP kwenye sehemu za mizozo, ikiwemo Syria, Iraq, Sudan Kusini na Yemen.