Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali watumieni vijana kujenga amani na ustawi duniani:Ban

Serikali watumieni vijana kujenga amani na ustawi duniani:Ban

Ingawa matarajio ya amani yanaonekana kuwa mbali katika dunia ya sasa iliyokumbwa na mizozo na mapigano, bado ndoto ya amani inadunda katika maisha ya watu kila pahali duniani.

Ni sehemu ya ujumbe wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon aliotoa kuelekea siku ya amani duniani tarehe 21 mwezi huu wa Septemba.

Ban amesema hakuna kundi linaloweza kufanikisha kufikia ndoto hiyo ya amani zaidi ya vijana ambao amesema kwa sasa ni wengi na hivyo..

“Viongozi wanapaswa kuwekeza kwa wajenzi wa amani vijana. Sote tunaweza kuimarisha amani. Mashirika ya kiraia, kampuni na hata taasisi za kidini wote wanaweza kujenga dunia yenye amani zaidi.”

Amesema ubia huo katika ujenzi wa amani ndio msingi wa ujumbe wa siku ya amani mwaka huu ambao ni ubia kwa amani utu kwa wote.

Katibu Mkuu amesema zama hizi ni za vitisho lakini pia ni zama za matumaini makubwa kwani siku chache viongozi wa dunia watakutana Umoja wa Mataifa kuridhia ajenda 2030 ambayo amesema ni hatua ya msingi inayoashiria maisha yenye utu kwa wote, ambako umaskini utasalia historian a amani itatamalaki.

Wakati huo huo, katika kuadhimisha siku hiyo hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ataongoza shughuli ya kugonga kengele ya amani kwenye bustani ya Umoja huo jijini New York, Marekani, ikiwa ni mojawapo ya shughuli za kuadhimisha siku ya amani duniani.