Wasanii wa Afrika watunga wimbo wa kuhamasisha jamii kuhusu maswala ya maendeleo

Wasanii wa Afrika watunga wimbo wa kuhamasisha jamii kuhusu maswala ya maendeleo

Katika kuelekea kuridhia malengo ya maendeleo endelevu mwisho wa mwezi Septemba, wimbo mpya uitwao “Tell Everybody” umezinduliwa hivi karibuni na kampeni ya Global Goals Afrika.

Wimbo huo ulitengenezwa na watayarishaji kutoka Kenya, David King Muthami, Msumbiji, Ellputo na Nigeria, Cobhams Asuquo, ukihusisha wasanii wa Afrika wakiwemo Diamond kutoka Tanzania, Mafikizolo kutoka Afrika Kusini na Sauti Sol kutoka Kenya.

Lengo la wimbo huo ni kuhamasisha hasa vijana washiriki zaidi katika maswala ya maendeleo na wawajibishe viongozi wa Afrika ili kutokomeza umaskini, kupambana na tofauti na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kulikoni? Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.