Harakati za kuwawezesha wanawake katika nafasi za maamuzi
Malengo ya maendeleo ya milenia MDGs, yanafikia ukomo wake mwezi huu mjini New York kwa kuwaleta pamoja wawakilishi wa nchi mbalimbali kutahimini utekelezaji wa malengo hayo na kisha kupitisha ajenda mpya ya maendeleo endelevu yaani SDGS au ajenda 2030.
Moja ya MDGs ni lengo namba tatu ambalo ni usawa wa kijinsia. Lengo hili linalenga mbali zaidi kwa kuangazia uwezeshaji wa wanawake na watoto wa kike katika nyanja mbalimbali ikiwamo za kisiasa.
Katika kuangazia hili nchi mbalimbali barani Afrika na kote duniani zinatoa fursa kwa wanawake kushika nafasi hizo . Mathalani, Rwanda ina rekodi ya pekee ya kinachoitwa hamsini kwa hamsini ambapo bunge la nchi hiyo lina idadi ya wanawake wabunge sawa na wanaume. Hali katika nchi nyingine barani humo ikoje? Tuanzie nchi jirani Uganda John Kibego anatujulisha..