Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumuiya ya kimataifa ionyeshe ukarimu kama Niger: Lanzer

Jumuiya ya kimataifa ionyeshe ukarimu kama Niger: Lanzer

Mkuu wa misaada ya kibinadamu katika ukanda wa Sahel, Toby Lanzer ametaka jumuiya ya kimataifa kuonyesha ukarimu kama unaoonyeshwa na nchi mathalani Niger zinazopokea wakimbizi wanaofurushwa kutoakana na machafuko ya kigaidi nchini Nigeria.

Akiongea mjini Geneva msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadmau OCHA Jens Larke amesema Bwana Lanzer amekaribisha juhudi zinazofanywa na wadau wa kibinadamu katika kusaidia mamalaka za kitaifa katika kubeba mzigo wa wakimbizi licha ya umaskini wa jamii wenyeji.

Msemaji huyo wa OCHA alikuwa akitoa tathmini ya ziara ya siku tano ya mkuu huyo wa OCHA ukanda wa Sahel aliyoifanya nchini Niger na kujionea hali nchini humo ambapo anasema

(SAUTI LARKE)

‘‘Akiwa kambini Lanzer amekutana na wanawake na watoto ambao wamemueleza kukatishwa tamaa kwa kuwa wamekosa makazi mara kadhaa hususani vijana ambao hawana matarajio na mustakabli wa elimu yao.’’

Kwa mujibu wa Lanzer Niger inahifadhi wakimbizi wa ndani 220,000 wengi wao wakiwa nikutoka Nigeria,Libya na Mali.