Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Feltman ahutubia Baraza la usalama kuhusu Burkina Faso

Feltman ahutubia Baraza la usalama kuhusu Burkina Faso

Kufuatia mapinduzi ya kijeshi huko Burkina Faso, Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa na kikao ambapo wajumbe wamepokea taarifa kutoka kwa Mkuu wa masuala ya siasa kwenye umoja huo Jeffrey Feltman. Abdullahi Boru na maelezo kamili.

(Taarifa ya Abdullahi)

Kikao hicho kilikuwa cha dharura ambapo baada ya kukamilika wajumbe walitoa taarifa inayolaani kitendo hicho na kutaka Rais wa mpito Michel Kafando, Waziri Mkuu Isaac Zida na mafisa wengine wanaoshikiliwa waachiliwe huru mara moja na kwa usalama.

Halikadhalika wamesihi pande zote kuzingatia kalenda ya mpito hususan kufanyika wka uchaguzi huru na wa haki wa wabunge na Rais tarehe 11 mwezi ujao.

Wajumbe hao wa Baraza la usalama pia wameelezea kuunga kwao mkono jitihada za wadau wote za kurejesha kipindi cha mpito nchini Burkina Faso ikiwemo zile za  mwakilishi maalum wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Afrika Magharbi, Mohamed Ibn Chambas,  jumuiya ya uchumi wa nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS  na Muungano wa Afrika.