Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna dalili njema kuelekea COP 21 : Jonas

Kuna dalili njema kuelekea COP 21 : Jonas

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekaribisha uwasilishwaji wa mikakati kutoka nchi wanachama katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi, mikakati ianayoelezwa kujenga msingi kuelekea katika mkutano wa makubaliano kuhusu mabadiliko ya tabianchi, COP 21, utakaofanyika mjini Paris mwezi Disemba.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York, msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu mabadiliko ya tabianchi na ajenda ya maendeleo endelevu Janos Pasztor amesema ni nchi 62 tu hadi sasa ambazo zimewasilisha mikakati yao na hivyo kuzitaka nchi nyingine kufanya hivyo.

Amesema kuna dalili njema ikiwa ni miezi miwili kabla ya COP 21

(SAUTI JANOS )

‘‘Tunaona kasi inajengwa, kujumuishwa kunajengeka pia na hatua zinachukua kasi. Kuna kila dalili njema za mafanikio ya mkutano wa Paris Desemba mwaka huu.’’

Kwa upande wake mshauri wa Katibu Mkuu kuhusu mipango baada ya 2015 Bi Amina Mohamed amewaambia waandishi wa habari kuwa mkakati wa maendeleo endelevu unahusisha kutowaacha nyuma wanawake akitolea mfano katika elimu hususani kwa vigori ambapo amesema lengo hilo halikutumia sawasawa na hivyo juhudi zaiodi zinahitajika.