Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti ya sasa ya UNCTAD ni tofauti na za awali : Kituyi

Ripoti ya sasa ya UNCTAD ni tofauti na za awali : Kituyi

Katibu Mkuu wa shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa UNCTAD Mukhisa Kituyi amesema ripoti mpya ya kila baada ya miaka minne  iliyozinduliwa  mapema wiki hii inakwenda sambamba na  mipango ya maendeleo endelevu SDGs inayotarajiwa kupitishwa hivi karibuni na nchi wanachama.

Katika mahojiano na Grace Kaneiya wa idhaa hii Bwana Kituyi amesema pia ripoti hiyo pia inaeleza kuhusu kuimarisha uzalishaji ili kuimarisha mifumo ya kiuchumi. Kwanza anaanza kuelzea kilichomo ndani ya ripoti.

(SAUTI MAHOJIANO)