Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yalaani mauaji ya mwanahabari wa Colombia, Flor Alba Núñez Vargas

UNESCO yalaani mauaji ya mwanahabari wa Colombia, Flor Alba Núñez Vargas

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Irina Bokova, amelaani leo mauaji ya mwanahabari wa Colombia, Flor Alba Núñez Vargas katika mji wa Pitalito, kusini mwa Colombia, mnamo Septemba 10.

Akilaani mauaji hayo, Bi Bokova amesema vyombo huru vya habari na jamii huru huenda bega kwa bega, na kwamba mashambulizi dhidi ya moja hudhoofisha nyingine.

Ametoa wito kwa mamlaka za Colombia kufanya kujitahidi kuchunguza uhalifu huo na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria.

Bi Flor Alba Núñez Vargas aliuawa mbele ya jengo la stesheni ya La Preferida Esteroradio, ambako alitangaza kipindi cha habari kila siku.