Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiukwaji mkubwa wa haki ulifanyika Sri Lanka: Ripoti

Ukiukwaji mkubwa wa haki ulifanyika Sri Lanka: Ripoti

Ripoti iliochapishwa leo na Umoja wa Mataifa imebainisha mfumo wa ukiukaji wa haki za kibinadamu uliokithiri nchini Sri Lanka kati ya 2002-2011, huku ikidhiirisha uwezekano wa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu kutekelezwa na pande zote mbili katika mgogoro.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa , Zeid Ra'ad Al Hussein, ameelezea umuhimu wa kuanzishwa kwa uchunguzi ili kuhakikisha maelfu ya watu walioteswa, walionyanyaswa kingono sawa na walioshambuliwa kwa makombora bila kujali wanapata haki.

Kamishna Zeid amesema, cha msingi ni uchunguzi wa mseto mahakamani ambao utawahusisha majaji wa kimataifa na kitaifa katika uchunguzi huo.

(Sauti ya Zeid)

"Lakini ni dhahiri kwamba mamlaka ya kisheria ya Sri Lanka haiana uwezo wa kukabiliana na uhalifu wa aina hii, kwanza hamna mbinu za kulinda wahanga na mashahidi, pili ni uhaba wa kisheria wa kukiabiliana na uhalifu wa makosa ya jinai ya aina hiyo, tatu ni kiwango ambacho sekta ya usalama na sheria imedhoofishwa na ufisadi kufuatia karne ya mizozo na kutowajibishwa.”