Ripoti ya UNCTAD imekuja wakati muafaka kuelekea SDGs:Kituyi
Katibu Mkuu wa Shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNCTAD Dkt. Mukhisa Kituyi amesema ripoti ya shirika hilo imekuja wakati muafaka ambapo nchi zinatarajiwa kuridhia maendeleo endelevu SDGs, baadaye mwezi huu.
Akihojiwa na Idhaa hii baada ya uzinduzi wa ripoti hiyo iitwayo “Kutoka maamuzi hadi hatua”amesema ni mujarabu kwani inataja mambo manne muhimu ikiwemo kuimarisha uzalishaji ili kubadilisha mifumo ya kiuchumi na kuimarisha ufanisi wa mataifa na masoko huku akitaja mikakati ya kufanikisha utekelezaji wa SDGs na kutokomeza umaskini uliokithiri.
(Sauti ya Kituyi)
Ripoti hiyo ya UNCTAD hutolewa kila baada ya miaka minne.