Misitu yatajwa kama sehemu muhimu ya kuwezesha maisha
Inakadiriwa kwamba takriban watu Bilioni 2.4 kote ulimwenguni wanategemea misitu kwa ajili ya huduma mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa chakula , kuni, mbao, dawa na ajira bila kusahau kuwa ni chanzo cha kipato. halikadhalika, muhimu kwa maisha ya theluthi moja ya watu ambao wanaishi vijijini na mijini vilevile, wanawake kwa waume, vijana kwa wazee.
Ni kwa mantiki hiyo ambapo kongamano la kumi na nne kwa ajili ya mustakabhali bora wa misitu liliwaleta pamoja viongozi na wadau mbalimbali ili kukubaliana njia bora za kulinda misitu wakati huu wa kuelekea kuridhia malengo ya maendeleo endelevu, SDG. Basi ungana na Grace Kaneiya katika makala hii.