Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali zinazojiamini hutoa fursa ya demokrasia kwa raia: Ban

Serikali zinazojiamini hutoa fursa ya demokrasia kwa raia: Ban

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya demokrasia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemulika maudhui ya mwaka huu yakiwa ni nafasi ya jamii, akilinganisha jamii na oksijeni kwenye demokrasia bila hiyo itakufa. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Katika ujumbe wake alioutoa kwa njia ya video, Bwana Ban amesema kwenye nchi zenye demokrasia imara, jamii na serikali zinashirikiana kwa ajili ya kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Nchi inayojiamini inawapa raia nafasi ya kujieleza na kushiriki kwenye maendeleo ya nchi. Jamii ina jukumu la msingi katika kuwajibisha serikali, na kuwakilisha mahitaji mbalimbali ya wananchi, wakiwemo wali wanaoteseka zaidi.”

Amesisitiza umuhimu wa kuendelea kulinda nafasi ya jamii wakati ambapo idadi kubwa zaidi ya serikali zinajaribu kuzuia kazi ya asasi za kiraia na uhuru wa jamii unapungua.