Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA yasikitishwa na ufurushaji wa wakimbizi wa ndani Bangui

OCHA yasikitishwa na ufurushaji wa wakimbizi wa ndani Bangui

Mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, Aurélien A. Agbénonci na wadau wa kibinadamu nchini humo, wameeleza kusikitishwa na kufurushwa kwa wakimbizi wa ndani 114 kutoka kituo cha Saint Jean Gabaladja mjini Bangui, mnamo Septemba 12.

Bwana Agbénonci amesema kuhamishwa kwa watu waliolazimika kuhama makwao ni lazima kufanyike kwa misingi ya uamuzi wa hiari ya watu hao, kuhakikisha mazingira bora ya usalama, kuheshimu utu wao, na kufuata  kanuni za sheria ya kimataifa ya kibinadamu na mkataba wa Kampala. Jens Laerke ni msemaji wa OCHA, Geneva…

“Kuna vituo tisa vinavyokabiliwa na tishio la kufurushwa kwa wakimbizi wa ndani, vikiwa vinawapa hifadhi wakimbizi zaidi ya 2,700 ambao huenda wakakabiliwa na hatma kama ya wale 114. Kwa ujumla, bado kuna vituio 31 vya wakimbizi wa ndani mjini Bangui, vikiwa na wakimbizi zaidi ya 27,000.”