Skip to main content

Tunahitaji vijana ili kutimiza malengo ya maendeleo endelevu- Ban

Tunahitaji vijana ili kutimiza malengo ya maendeleo endelevu- Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema leo kuwa wakati serikali zikijiandaa kupitisha ajenda mpya ya maendeleo endelevu ili kuleta mabadiliko kwa maisha ya watu wote ifikapo mwaka 2030, mchango wa vijana unahitajika ili kutimiza malengo hayo.

Ban amesema hayo katika ujumbe wake kwa kongamano la vijana, ambao amesema walisaidia katika kubuni ajenda hiyo kabambe.

Katibu Mkuu amesema malengo ya maendeleo endelevu yanashughulikia changamoto kubwa za kizazi cha sasa, zikiwemo kupata elimu bora, ajira, kutiokomeza unyanyasaji na kulinda mazingira, na kwamba ulimwengu unawahitaji vijana na nguvu zao, mawazo yao na mikakati yao ili kutimiza malengo hayo.