Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita na Amani: michoro ya mita 14 yazinduliwa New York

Vita na Amani: michoro ya mita 14 yazinduliwa New York

Michoro iitwayo “War and Peace”, yaani Vita na amani, iliyotengenezwa na mchoraji wa Brazil marehemu Claudio Portinari imerejeshwa wiki hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa baada ya kutembezwa kwa miaka michache nchini Brazil na Ufaransa.

Michoro hiyo miwili mikubwa kabisa yenye urefu wa mita 14 iliwekwa awali mwaka 1957 kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani kwa ajili ya kukumbusha viongozi wa dunia kuhusu mateso yanayosababishwa na vita na pia kuhusu ndoto ya amani ya kimataifa.

Hafla maalum ilifanyika awali wiki hii kwa ajili ya uzunduzi upya wa michoro hiyo, ambapo muziki na video zilizochezwa zimeonyesha umuhimu wa kuendelea kuwa na ndoto hiyo ya amani. Ungana na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.