Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania yaijulisha WHO kuhusu mlipuko wa kipindupindu, DSM yaongoza

Tanzania yaijulisha WHO kuhusu mlipuko wa kipindupindu, DSM yaongoza

Wizara ya Afya na Jamii nchini Tanzania, imelijulisha Shirika la Afya Duniani, WHO kuhusu mlipuko wa kpindupindu nchini humo ambapo idadi ya vifo imeongezeka na kufikia 14 huku wagonjwa waliothibitika wakiwa ni 1268. Amina Hassan na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Amina)

WHO imepatiwa taarifa hizo leo huku Mkurugenzi Msaidizi wa kitengo cha udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kwenye wizara ya afya nchini Tanzania, Dkt. Janeth Mghamba akieleza Idhaa hii mikoa iliyoathirikazaidi.

(Sauti ya Dkt.Mghamba)

Amesema tayari wameunda kikosi kazi cha kitaifa cha kusaidia udhibiti na kinga dhidi ya Kipindupindu lakini changamoto hasa Dar e salaam ni..

(Sauti ya Dkt. Mghamba)

Licha ya mlipuko huko WHO imesema haitoi ushauri wowote wa zuio la safari au biashara na Tanzania kwa kuzingatia taarifa za sasa zilizopo kuhusu mlipuko huo.