Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kila mtu ni mzee mtarajiwa, wekeni sera za kuboresha ustawi wa wazee:

Kila mtu ni mzee mtarajiwa, wekeni sera za kuboresha ustawi wa wazee:

Wakati lengo namba tatu la maendeleo endelevu, SDGs linataka kuhakikisha afya bora na ustawi kwa watu wenye umri wote, nchini Kenya serikali na jamii imeombwa kuangazia ustawi wa wazee ambao baadhi yao wanakumbwa na madhila ikiwemo kukosa pensheni, malezi na hata matibabu.

Akihojiwa na idhaa hii baada ya kuhutubia mkutano ulioangazia athari za SDG kwa wazee, mwanaharakati wa haki za wazee kutoka Kenya Esther Wamera amesema hata cha kustajabisha Kenya haipo kwenye ripoti mpya ya Helpage International kuhusu masuala ya uzee na hiyo inadhihirisha kutopatiwa kipauembele kwa masuala hiyo kwa kuwa..

(Sauti ya Wamera)

Katika ripoti hiyo ni nchi 96 tu kati ya 194 ndio ziliwasilisha ripoti kuhusu hali ya ustawi wa wazee ambapo kwa ujumla Uswisi ndio mahala bora zaidi kwa ustawi wa wazee duniani huku kwa bara la Afrika Mauritius ikiibuka kidedea.

Nchi yenye ustawi duni zaidi ni Afghanistan ambayo ilishika nafasi ya 96.