Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake wamesimama kidete kunasua watoto wao kutoka ugaidi:

Wanawake wamesimama kidete kunasua watoto wao kutoka ugaidi:

Siku ya Jumatano katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kamati ya baraza la usalama kuhusu udhibiti wa ugaidi na misimamo mikali ilikuwa na kikao cha kupatiana taarifa juu ya  harakati hizo. Wanawake watatu kutoka Iraq, Nigeria na Kenya walikuwa miongoni mwa wazungumzaji wakuu wakieleza kile ambacho mashirika yao yanafanya kusaidia kukwamua nchi zao kutokana na wimbi la vitendo vya ugaidi na misimamo mikali vinavyotishia usalama wa jamii, taifa na dunia kwa ujumla. Kutoka Kenya Sureya Roble-Hersi ambaye ni Makamu wa pili wa Rais wa shirika la Maendeleo ya wanawake ndiye alikuwa mzungumzaji na kabla ya kikao hicho alihojiwa na Assumpta Massoi wa idhaa hii akieleza kile wanachofanya, masahibu yanayokumba vijana wanaporudi kutoka Somalia na hata kinachowatia moyo wanawake hao. Anaanza kwa kuelezea wanakoendesha shughuli zao na kile kilichowasukuma kuingia katika masuala ya usalama.