India yaongoza kwa binadamu kutumia viuadudu kujiua:WHO

10 Septemba 2015

Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kupinga vitendo vya kujiua Shirika la Afya Duniani WHO limeeleza kuwa idadi ya watu wanaojiua inazidi idadi ya watu wanaokufa kutokana na vita na mauaji. Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Kwa mujibu wa WHO, ni watu zaidi ya 800,000 wanaojiua kila mwaka, asilimia 75 ya vifo hivi vikitokea kwenye nchi zenye kipato cha kati au cha chini.

Njia tatu zinazotumiwa zaidi kujiua zikiwa ni matumizi ya dawa za kuua wadudu au viuadudu, kujinyonga na kujipigia risasi, ambapo WHO inataka nchi zichukue mikakati ya kuzuia vitendo hivyo, ikiwemo kudhibiti upatikanaji wa njia hizo.

Mathalani nchini India, ambako viuadudu vinatumiwa sana kwenye sekta ya kilimo vijijini, tayari WHO imesaidia kujenga ghala ya kukusanya viuadudu ili visipatikane kwenye kila nyumba. Hatua hiyo imewezesha kupungua kwa idadi ya vifo kwa kiasi kikubwa kwenye vijiji ambako mradi huo umetekelezwa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter