Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya visa vya Ebola yapungua, WHO yaendelea kuwa makini

Idadi ya visa vya Ebola yapungua, WHO yaendelea kuwa makini

Mwakilishi maalum wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO kwa ajili ya Ebola, Bruce Aylward, amesema ametiwa moyo na taarifa za kupungua kwa idadi ya visa vya Ebola.

Hata hivyo jitihada za kupambana na Ebola zinaendelea, ameeleza Bwana Aylward akiongea na waandishi wa habari leo mjini Geneva Uswisi baada ya kumaliza ziara ya siku kadhaa kwenye ukanda wa Afrika Magharibi uliokumbwa na Ebola,

“ Hayo yote yameanza na kisa kimoja. Na tunapaswa kufikia huko, tena na tena na tena. Wiki iliyopita, tulikuwa na visa viwili tu, wiki moja kabla visa vitatu tu, lakini kila kisa ni hatari ya kurudia kwenye hali mbaya sana, iwapo hakitadhibitiwa.”

Daktari Aylward amesema Umoja wa Mataifa unatarajia kuzindua hatua ya tatu ya operesheni za kupambana na Ebola ikiwa ni kuwezesha mamlaka za serikali za nchi husika kuendelea kudhibiti hali ya mlipuko nchini kote na kufuatilia manusura ambao wanaweza kuendelea kuambukiza wenzao.