Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana wanaorejea baada ya kulaghaiwa na ugaidi wahitaji msaada

Vijana wanaorejea baada ya kulaghaiwa na ugaidi wahitaji msaada

Ushiriki wa wanawake katika kupatia suluhu ugaidi na misimamo mikali ni jambo lisiloepukika wakati  huu ambapo siyo tu wavulana wanajitumbukiza kwa hiari kwenye ugaidi bali pia wasichana na hata wanawake.

Hayo yamesemwa na Sureya Roble-Hersi, Makamu wa pili wa mwenyekiti wa shirika la Maendeleo ya wanawake nchini Kenya alipohojiwa na Idhaa hii kando mwa kikao kuhusu nafasi ya wanawake kudhibiti ugaidi na misimamo mikali mjini New York, Marekani, akitolea mfano Mombasa ambako  ulaghai unaathiri vijana na kuingia kwenye zahma hiyo.

(Sureya-1)

Lakini amesema vijana baada ya kubaini kuwa ahadi waliyopatiwa si ya kweli hurejea nyumbani na kutengwa na hivyo ombi lao kwa serikali ni..

(Sureya-2)

Shirika la Maendeleo ya wanawake Kenya linaendesha programu zake za kudhibiti ugaidi kwenye maeneo ya Mombasa, Garissa na Eastleigh jijini Nairobi.