Kasi ya migawanyiko duniani inaongezeka kila uchao: Ban

9 Septemba 2015

Dunia inasonga mbele kwa kasi kubwa sana, halikadhalika migawanyiko miongoni mwa watu pamoja na chuki, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wakati akihutubia kikao cha hali ya juu kuhusu utamaduni wa amani kilichofanyika leo jijini New York Marekani.

Kikao hicho kilichoitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kimefanyika wakati ambapo Ban amesema chuki baina ya watu wa imani mbali mbali za dini, jinsia na hata makabila zinashamiri kila uchao na kusababisha watu kuhama makwao akitolea mfano Syria.

Amesema kinachomchosha zaidi ni wale wanaofanya mashambulio kwa kisingizio cha dini wakidai kile wanachosema ni utukufu wakati ni kujiletea aibu. Katibu Mkuu amesema anachoangalia sasa ni vijana Bilioni 1.8 duniani ambao wanahaha kusaka amani kwa ajili ya maendeleo akisema….

(Sauti ya Ban)

“Ndio maana natoa wito wa kuwapatia vijana nafasi kwenye meza ya mazungumzo. Ni wakati wa kuwekeza kwa vijana kama wajenzi wa amani. Wanaweza kuwa na mchango mkubwa katika utulivu wa kudumu.”

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter