Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Harakati za ulinzi wa kulinda misitu ya asili Tanzania

Harakati za ulinzi wa kulinda misitu ya asili Tanzania

Mkutano wa 14 kuhusu misitu unaendelea mjini Durban nchini Afrika Kusini, ukiwa ni mkutano wa kwanza kufanyika barani Afrika ukiwaleta pamoja watu kutoka nchi na maeneo mbalimbali ikwemo serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kwa ajili ya kuchangia katika maswala ya misitu na kujadili maendeleo endelevu.

Moja ya ajenda ni kuhusu kuangalia mustakhabali wa misitu endelevu wakati huu ambako nako nchini Tanzania kumefanyika mkutano ambao ulikuwa na lengo la kujadili mambo muhimu kabla ya mkutano wa Paris Ufaransa baadaye mwaka huu, COP 21 utakaopitisha mkataba mpya wa mabadiliko ya tabianchi. Katika mkutano huo nchini Tanzania,  Stella Vuzo , afisa wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa amezungumza na mshiriki kutoka Shirika lisilo la kiserikali nchini humo, Mpingo, Glory Masau  akianza kwa kuelezea shirika lake linachokifanya.