Skip to main content

Cheikh Ahmed asikitishwa na kufunuliwa kwa nyaraka za UM Yemen

Cheikh Ahmed asikitishwa na kufunuliwa kwa nyaraka za UM Yemen

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Yemen, Ismail Ould Cheikh Ahmed, ameeleza kusikitishwa na ripoti za vyombo vya habari kuhusu ufunuzi wa mawasiliano ya ndani ya Umoja wa Mataifa.

Taarifa ye msemaji wa Katibu Mkuu imesema kuwa yaliyomo katika ripoti hizo, hususan katika vyombo vya habari vya Yemen na mitandao ya intaneti, ni uongo mtupu na ufafanuzi mbaya.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa ripoti hizo hazionyeshi msimamo mjumbe maalum wa Katibu Mkuu au ule wa Umoja wa Mataifa, na kwamba mjumbe huyo maalum ataendelea na juhudi zake za kufanya mashauriano na pande kinzani za Yemen ili kufikia suluhu la kudumu la amani.