Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ladsous azindua eneo bila silaha huko Bambari, CAR

Ladsous azindua eneo bila silaha huko Bambari, CAR

Mkuu wa Idara ya Operesheni za Kulinda Amani za Umoja wa Mataifa Hervé Ladsous ametangaza kuzindua eneo maalum mjini Bambari nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ambalo halitaruhusiwa kuwa na silaha kuanzia leo.

Bwana Ladsous amesema hayo akiongea na waandishi wa habari akiwa ziarani nchini humo, akisema Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini CAR, MINUSCA, umeamua kuandaa eneo kama hilo ili kuraisisha shughuli za raia na kulinda usalama wao, pia kuraisisha kazi za wahudumu wa kibinadamu.

“ Nataka kusisitiza kwamba nafurahia kuwa vikundi vya waasi wamejituma kuheshimu uamuzi huo. Lengo kuu ni kuimarisha usalama wa raia, na kuandaa mazingira yatakayowezesha wakimbizi wa ndani kurudi kwao, pia kuwezesha uandikishaji wa wapiga kura ambao unaanza tarehe 14, Septemba.”

Uamuzi huo unafuata wito uliotolewa na wakazi wa Bambari walioomba kulindwa dhidi ya ghasia kutoka kwa waasi kwenye eneo hilo.

Ziara ya Bwana Ladsous ya siku nne nchini CAR imefanyika wakati ambapo serikali inaandaa uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu,