Viongozi wa kidini watazamia kuzindua mwongozo wa maendeleo endelevu

8 Septemba 2015

Dini nane kubwa duniani zinatazamiwa kuzindua mipango kabambe ya kusaidia kunyanyua mamilioni ya watu kutoka kwa umaskini, sambamba na malengo ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu (SDGs).

Mipango hiyo ambayo Shirika la Mfuko wa Idadi ya Watu, UNFPA limetaja kuwa baadhi ya ahadi halisi zaidi kufikia sasa, itazinduliwa katika mkutano wa viongozi wa imani mbali mbali unaoanza leo mjini Bristol, Uingereza.

Mkutano huo umeandaliwa na Umoja wa Mataifa, kutokana na utambuzi kuwa dini ni kitu muhimu kwa asilimia 80 ya watu kote duniani, kama Mchungaji Charles Odira alivyoeleza katika mahojiano na idhaa hii.

(Sauti ya Fr. Charles)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter