Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serena, Neymar na Kolo Toure wachagiza SDGs

Serena, Neymar na Kolo Toure wachagiza SDGs

Mabalozi wema watatu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF leo wameungana na kampeni ya kuzindua kampeni ya kuelimisha watoto katika nchi zaidi ya 100 duniani kuhusu malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Mabalozi hao ni bingwa nambari moja wa tenisi duniani kwa wanawake Serena Williams, na wasakata kabumbu mashuhuri Kolo Toure na Neymar.

Taarifa ya pamoja ya UNICEF na Global Goals, imesema kupitia mfumo huo watoto watafahamu changamoto zinazokabili jamii yao kama vile mazingira, umaskini na kushiriki kujenga mustakhbali.

Mpango h uo wa kuelimisha watoto utahusisha masomo darasani kwenye mabara yote duniani kwa wiki ya kuanzia tarehe 28 mwezi huu ambapo wasichana na wavulana 500 wenye umri wa kati ya miaka Nane hadi 14 watapatiwa fursa ya kuelimisha malengo hayo.

Masomo hayo yatatolewa na viongozi wa serikali na mawaziri kutoka nchi mbali mbali ambapo mtunzi mashuhuri wa filamu duniani, Richard Curtis amesema ni fursa nzuri ya watoto kufahamu malengo hayo ili wawe sehemu ya kufanikisha utekelezaji wake.