Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msanii wa Nigeria, D’Banj apigania usawa wa jinsia kupitia muziki

Msanii wa Nigeria, D’Banj apigania usawa wa jinsia kupitia muziki

Benki ya Dunia ilizindua mapema mwaka huu mfululizo wa makala uitwao “Muziki kwa maendeleo”. Kupitia mfululizo huo wa makala zinazowekwa kwenye tovuti yake, Benki ya dunia inawapa fursa wasanii kutoka kote duniani wanaohusika katika masuala ya maendeleo kushirikisha muziki wao na kuzunumzia masuala yanayowagusa zaidi.

Mmoja wa wasanii hao ni nyota wa Nigeria, D’Banj. Ungana basi na Joshua Mmali akikuletea kionjo cha kampeni ya D’Banj ya kupigania usawa wa jinsia kupitia muziki.