GBC ya Kenya yaibuka kidedea shindano la teknolojia

GBC ya Kenya yaibuka kidedea shindano la teknolojia

Kampuni moja nchini Kenya imeibuka kidedea katika shindano la kampeni ya kuanzisha mfumo wa digitali wa kuunganisha mtandao wa wajasiriamali wanawake Milioni Moja na masoko. Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Greenbell Communications, GBC ilikuwa miongoni mwa kampuni 300 zilizoingia kwenye shindano hilo lililoandaliwa na kituo cha biashara duniani, ITC, Google na CI&T ambapo washindi walitangazwa mwishoni mwa maonyesho na jukwaa la wafanyabiashara wanawake huko Sao Paulo Brazil.

ITC ilizindua mpango wa mtandao wa wanawake wajasiriamali na masoko mwezi Septemba mwaka huu ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Arancha Gonzalez amesema ubunifu wa mfumo huo wa kidigitali utarahisisha kuunganisha mtandao huo wa wafanyabiashara na masoko ya bidhaa zao.

Sasa GBC itawasilisha muundo wao ulioshinda kwenye jukwaa la dunia la maendeleo ya biashara ya nje huko Doha Qatar, tarehe 20 na 21 mwezi ujao.