Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mazungumzo ya kisiasa kuhusu Libya yaingia siku ya pili

Mazungumzo ya kisiasa kuhusu Libya yaingia siku ya pili

Mazungumzo ya kisiasa kuhusu Libya yameingia siku yake ya pili hii leo mjini Geneva, yakilenga kukamilisha mashauriano kuhusu makubaliano ya kisiasa na masuala mengineyo, ikiwemo kuunda serikali ya mkataba wa kitaifa.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva Ahmad Fawzi, amesema kuwa Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Libya, Bernardino Leon, amekuwa na mikutano kadhaa na washiriki mbalimbali wa mazungumzo hayo usiku na mchana tangu jana Alhamis, na anafanya mikutano mingine leo.

“Wawakilishi wa pande zote zilizoalikwa wapo Geneva, na wanashiriki awamu hii ya mazungumzo. Wanajumuisha wawakilishi wa bunge na baraza la kitaifa kwa ujumla.”