Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ushrikishswaji wa mabunge katika kutekeleza SDGs ni kiungo muhimu:Spika Muturi

Ushrikishswaji wa mabunge katika kutekeleza SDGs ni kiungo muhimu:Spika Muturi

Wakati mkutano wa maspika wa mabunge ukiwa umehitimishwa jijini New York, Marekani, kumetolewa wito wa kuwasaidia watu kutimiza ndoto zao wakati huu ambapo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimeafikiana malengo mapya ya maendeleo endelevu yatakayoridhiwa baadaye mwezi huu.

Kwa upande wake mwakilishi wa Kenya katika mkutano huo wa maspika, spika wa bunge la taifa Justin Muturi katika mahojiano na Grace Kaneiya wa Idhaa hii pindi tu baada ya kuwasilisha ripoti yake kwa kongamano hilo amesema kwamba mabunge yana nafasi kubwa katika kuhakikisha kwamba malengo enelevu yanatekelezwa. Hapa anaanza kwa kueleza ujumbe wake kwa mkutano huo wa Nne.