Mkuu wa Haki za binadamu alaani madai mapya ya unyanyasaji wa kingono CAR

Mkuu wa Haki za binadamu alaani madai mapya ya unyanyasaji wa kingono CAR

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Zeid Ra’ad Al Hussein, ambaye yupo ziarani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, amelaani vikali madai mapya ya unyanyasaji wa kingono uliofanywa na vikosi vya walinda amani nchini humo. Taarifa zaidi na John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo waligundua mnamo Alhamis, Agosti 30, kuwa msichana mmoja barubaru alidaiwa kunyanyaswa kingono na askari wa vikosi vya Ufaransa viitwavyo Sangaris. Msichana huyo alijifungua mnamo mwezi Aprili mwaka huu.

Kamishna Zeid amekitaja kitendo hicho kama cha karibuni zaidi katika msururu wa madai ya unyanyasaji wa kingono unaofanywa na vikosi vya kigeni nchini CAR.

Ameongeza kuwa ni lazima njia zipatikane za kuzuia vitendo kama hivyo alivyotaja kuwa vya machukizo, kufanywa na askari ambao wanapaswa kuwalinda raia walio hatarini popote pale.

Cecile Pouilly, ni msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu..

(Sauti ya Cecile)

“Kimsingi, askari hawa wanapelekwa kuwalinda raia, na wanachofanya ni kwamba, wanatumia vibaya nafasi zao za mamlaka, na wanajikuta wakiwanyanyasa hata watoto walio chini ya umri.”