Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Visa Tisa vipya vya homa ya matumbo vyashukiwa Yalda

Visa Tisa vipya vya homa ya matumbo vyashukiwa Yalda

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi wa kipalestina, UNRWA limesema katika harakati zake za matibabu kwa wagonjwa 330 huko Yarmouk, kwenye mji mkuu wa Syria, Damascua, lina shuku ya kuwepo kwa wagonjwa Tisa wa homa ya matumbo.

Matibabu hayo yanaendelea katika kituo cha tiba kilichoanzishwa huko Yalda ambako kuongezeka kwa kiwango cha joto na ukosefu wa mara kwa mara wa maji na vyakula unazidi kuathiri raia.

Maafisa wa afya wa UNRWA wanasema hali inazidi kuwa mbaya kwa raia hao na hivyo kusema kipaumbele cha shirika hilo ni kutoa misaada ya kibinadamu kwa wahitaji ndani  ya kambi ya Yarmouk na kuhakikisha kuna mazingira salama ili misaada hiyo iweze kufikishwa.

Zaidi ya asilimia 95 ya wakimbizi wa kipalestina wanategemea UNRWA katika kukidhi mahitaji yao ya kila siku ikiwemo maji, chakula na afya wakati huu ambapo kambi yao imezingirwa kutokana na mapigano nchini Syria.