Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati kuhusu ulinzi wa wafanyakazi wahamiaji yamulika hali Guinea

Kamati kuhusu ulinzi wa wafanyakazi wahamiaji yamulika hali Guinea

Kamati kuhusu ulinzi wa haki za wafanyakazi wahamiaji na jamaa zao imemulika leo hali nchini Guinea, ikizingatia ripoti ya taifa hilo la Afrika Magharibi kuhusu utekelezaji wa mkataba wa kimataifa kuhusu ulinzi wa wafanyakazi wahamiaji na familia zao.

Akiiwasilisha ripoti hiyo, Waziri wa Haki za Binadamu na Uhuru wa Kiraia nchini Guinea, amesema Guinea iliridhia mkataba huo mwaka 2000, na kwamba licha ya matatizo ya kimfumo, nchi yake imejikita kikamilifu katika kulinda haki za wafanyakazi wahamiaji na familia zao. Amongeza kuwa nchi hiyo ilipitisha sheria ya kazi ya mwaka 2014, ambayo inapinga ubaguaji kwa misingi kadhaa katika ajira.

Katika mjadala uliofuata, wataalam wa haki za binadamu wamesisitiza kuwa ukosefu wa takwimu zipasazo na takwimu duni kuhusu wahamiaji na watu nchini humo kwa ujumla ni dosari kubwa ambayo inapaswa kurekebishwa.

Mtaalam wa kamati hiyo kuhusu Guinea, Khedidja Ladjel, amesema suluhu linaweza kupatikana katika kuweka sera mwafaka za uhamiaji, ambazo zitamwezesha kila mtu kutimiza ndoto na uwezo wake.