Skip to main content

Mazungumzo yanaonyesha dalili njema za muafaka: UNSMIL

Mazungumzo yanaonyesha dalili njema za muafaka: UNSMIL

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya na mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNSMIL Bernardino Leon amewaambia waandishi wa habari mjini Istanbul Uturuki kuwa amekamilisha mazungumzo na wawakilishi wa congress ambayo yanaonyesha dalili njema za maridhiano.

Katika mkutano huo Bwana Leon amesema jambo muhimu katika mchakato endelevu wa mazungumzo ni utiwaji saini wa makubalino ili kuanza kuyatekelza ifikapo mwezi Oktoba .

Amesema kinachofanyika sasa ni kushughulikia viambatisho na kufanya kazi na serikali ili kufikia mwisho utakaoleta maana na kusainiwa na kila mtu ili kuelekea katika makubaliano

Mkuu huyo wa UNSMIL amesema ndani ya wiki mbili hadi tatu wanatarajia kufikia suluhu la mgogoro nchini Libya