Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ifikapo 2020 Gaza kutakuw ahakufai kuishi: UNCTAD

Ifikapo 2020 Gaza kutakuw ahakufai kuishi: UNCTAD

Mazingira ya kuishi huko Gaza yanaelezwa kuwa mabaya sana na hayafai kwa mwanadamu na kwamba ifikapo mwaka 2020 eneo hilo litakuwa halifai kuishi imesema ripoti ya shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNCTAD.

Shirika hilo limesema kuwa licha ya adha ya ukosefu wa maji na umeme, wakazi milioni 1.8 wa Gaza bado hawajapona majeraha ya uharibifu kufuatia machafuko ya mwaka jana kutoka Israel.

UNCTAD imesema kwamba ni wazi uchumi wa Gaza sasa umeshuka na kwamba machafuko ya mwaka jana yaliteketeza eneo hilo huku bado mashambulizi yakizidi kudidimiza jamii ya Gaza. Mahmoud Elkhafif ni afisa wa Gaza

(SAUTI MAHMOUD)

"Kutokana na ukweli kuwa kuna upungufu wa umeme, hospitali kadhaa zimetekezwa, hakuna maji ya kunywa, mwanadamu yeyote timamu anaweza kutilia shaka kitakachotokea. Namaanisha tulikuwa na utafiti kabla ya uharibifu wa mwaka 2014 ukionyesha kuwa Gaza itakuwa haifai kuishi mwaka 2020, sio kwamba mambo yalisalia kama yalivyo lakini yalikuwa mabaya zaidi mwaka 2014.’’

Kwa mujibu wa UNCTAD mwaka 2000 watu 72,000 walihitaji msaada wa chakula lakini idadi hiyo sasa imeongezeka hadi takribani milioni moja huku ukosefu wa ajira ukiwa asilimia 80 huko Gaza.