Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yawasilisha misaada ya kibinadamu kufuatia mapigano Agosti masahariki mwa Ukraine

UNHCR yawasilisha misaada ya kibinadamu kufuatia mapigano Agosti masahariki mwa Ukraine

Shirika la Kuhudumia Wakmbizi, UNHCR, limesema kuwa kwa mara ya kwanza katika majuma kadhaa, limeweza kufikisha misaada ya kibinadamu mashariki mwa Ukraine, Vifaa hivyo vya misaada ya kibinadamu vitazisaidia familia zaidi ya 5,000 kwa makazi na kufanyika ukarabati nyumba zao.

UNHCR imesema kuwa mwezi wa Agosti ulishuhudia mapigano mazito kaskazini mwa Donetsk, ndani na karibu na mji wa Horvlika.

Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR,

"UNHCR iliweza kuwasilisha misaada ya kibinadamu katika mji wa Horvlika na miji iliyo karibu ambayo haitawaliwi na serikali, hii ni mara ya kwanza tumeweza kuwasilisha msaada katika kipindi cha wiki chache, ambapo malori 13 yaliyobeba tani 260,00 ya vifaa vya makazi na mahitaji mengine muhimu yamewasilishwa. Licha ya kusainiwa makubaliano ya kusitisha mapigano mnamo Februari 2015, mapigano karibu na mji wa Horvlika yamesababisha uharibifu mwa maeneo ya makazi na kuwalazimu wakazi kukimbilia makazi ya chini ya ardhi  ya nyumba zao zilizoharibiwa."

Tangu kuanza mgogoro mnamo mwaka 2014, takriban asilimia 40 ya wakazi wa Horvlika wamehama makwao, na kulingana na mamlaka za mji huo, ni kati ya watu wapatao 150,000 na 200,000 tu ndio waliosalia katika mji huo.