Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akutana na maspika wa mabunge ya India

Ban akutana na maspika wa mabunge ya India

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa bunge la chini la India, Lok Sabha, Bi Sumitra Mahajan na Naibu Mwenyekiti wa bunge la ngazi ya juu la India, Rajya Sabha, Pallath Joseph Kurien.

Wakati wa mkutano huo, Bwana Ban amepongeza umahiri wa demokrasia ya India na kujadili masuala ya kipaumbele ya Umioja wa Mataifa kwa mwaka huu, likiwemo kuafikia mkataba wa maana na unaoheshimiwa kisheria kuhusu mabadiliko ya tabianchi, na kuridhia ajenda mpya ya maendeleo endelevu.

Katibu Mkuu amesisitiza mchango muhimu wa bunge la India katika kulinda haki za wanawake na kuendeleza usawa wa jinsia, ikiwemo kupambana na ukatili dhidi ya wanawake.