Skip to main content

Ban amkumbuka Jenerali Jaborandy Jr.

Ban amkumbuka Jenerali Jaborandy Jr.

Kifo cha Mkuu wa vikosi vya Umoja wa Mataifa vya kuweka utulivu nchini Haiti, MINUSTAH, Jenerali Jose Luiz Jaborandy Jr.  kimepokelewa kwa mshtuko mkubwa na Katibu Mkuu wa Umoja huo Ban Ki-moon.

Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu imemnukuu akimwelezea Jenerali Jaborandy, Jr. kama kiongozi mchapakazi aliyejitolea kwa ajili ya amani.

Ban ametoa shukrani kwa utendaji wa kiongozi huyo wakati wa uhai wake huku akituma salamu za rambirambi kwa familia yake na serikali ya Brazili ambako ndiko anatoka.

Jenerali Jaborandy Jr, amefariki dunia Agosti 30 akiwa safarini kwenye ndege kutoka Miami, Marekani akielekea Brazil.

Aliteuliwa kushika wadhifa huo mwezi Machi mwaka 2014.