Huduma za afya za dharura zinahitajika Yemen: WHO

31 Agosti 2015

Shirika la afya ulimwenguni WHO na washirika,  wanahaha kunusuru maisha ya mamilioni ya raia wanaoteseka kutokana na vita nchini Yemen na sasa juhudi zaidi zimeelekzwa katika kuhakikisha huduma za afya jimboni liitwalo Taiz ambako maelfu wanahataji huduma.

Katika mhojiano na idhaa hii Dr. Ahmad Shadou ambaye ni mwakilishi maalum wa WHO nchini Yemena anasema juhudi kubwa zinafanyika ili kulifikia jimbo hilo na kwa sasa majadiliano dhidi ya pande kinzani ili kuruhusu maeneo hayo kufikiwa yanaendelea.

Amesema wanatarajia hapo kesho watawasili jimboni Taiz na kuongeza.

(SAUTI DK AHMAD)

‘‘Kwa upande mwingine pia Umoja wa Mataiofa unaandaa msafara wa usaidizi huko Taiz. Msafara unatarajiwa kuondoka mjini Sana’a  alhamisi au ijumaa wiki hii, kwa ajili ya watu katika maeneo athirika huko Taiz.’’

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter