Huduma za afya za dharura zinahitajika Yemen: WHO
Shirika la afya ulimwenguni WHO na washirika, wanahaha kunusuru maisha ya mamilioni ya raia wanaoteseka kutokana na vita nchini Yemen na sasa juhudi zaidi zimeelekzwa katika kuhakikisha huduma za afya jimboni liitwalo Taiz ambako maelfu wanahataji huduma.
Katika mhojiano na idhaa hii Dr. Ahmad Shadou ambaye ni mwakilishi maalum wa WHO nchini Yemena anasema juhudi kubwa zinafanyika ili kulifikia jimbo hilo na kwa sasa majadiliano dhidi ya pande kinzani ili kuruhusu maeneo hayo kufikiwa yanaendelea.
Amesema wanatarajia hapo kesho watawasili jimboni Taiz na kuongeza.
(SAUTI DK AHMAD)
‘‘Kwa upande mwingine pia Umoja wa Mataiofa unaandaa msafara wa usaidizi huko Taiz. Msafara unatarajiwa kuondoka mjini Sana’a alhamisi au ijumaa wiki hii, kwa ajili ya watu katika maeneo athirika huko Taiz.’’